Habari za Punde

Waziri wa Biashara Masoko na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali Afungua Semina ya Mafunzo ya Mali Ubunifu Zanzibar.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amani Salum Ali akifungua Semina ya mafunzo ya Mali Bunifu iliowashirikisha Wadau Mbalimbali Zanzibar ilioandaliwa kwa pamoja na ARIPO,JPO,WIPO na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Ubalozi wa Japani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Mapindi Zanzibar.
Waziri Balozi Amina Salum Ali akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo ya Mali Ubunifu inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar.
Washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Biashara Viwanda Masoko Zanzibar Mhe Balozi Amani Salum Ali wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa ARIPO Fernando Dos Santos akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo ya Siku mbili ya Mafunzo kuhusiana na Mali Bunifu kwa Wadau mbalimbali Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar.
Balozi wa Japani Nchini Tanzania Yuji Nakayama akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo ya mafunzo na kutowa nasaha zake kwa washiriki wa mafunzio hayo yalioandaliwa  kupitia Taasisi za ARIPO, WIPO, JPO na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushiriki na Japan yanayofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania Yuji Yakayama akisisitiza jambo wakati akizungumza katika ufunuzi wa mafunzo hayo. 
Mwakilishi Kutoka Shirika Linalisimamia Masuala ya Mali Ubunifu Duniani (WIPO) Joyce Banya akizungumza wakati wa semina hiyo kwa Wadau wa maendeleo Zanzibar inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar. 
Washiriki wakifuatilia semina hiyo ya mafunzo wakati wa ufunguzi wake uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Malindi Zannzibar.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.