Makamu wa Rais wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka
kwa Mfanyakazi wa Kampuni ya Zantel alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika
maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba
yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Waziri wa
Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage na wa pili kushoto ni Meneja
wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia
Hassan Suluhu akifurahia jambo na wafanyakazi wa Zantel alipotembelea banda la
Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41
Makamu wa Rais wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akimpongeza Mratibu wa Masoko wa
Zantel-Zanzibar, Haji Khatib kwa kuchangia damu kwa hiari baada ya kiongozi
huyo kutembelea banda la kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma
mbalimbali zinazotolewa. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu
Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya
watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya
Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja
vya Mwl J.K Nyerere.
Makamu wa Rais wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri alipotembelea banda la
Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama
Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Makamu wa Rais wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel,
Hamza Zuheri (Katikati) alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya
41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika
viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel,
Rukia Mtingwa.
Makamu wa Rais wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel,
Rukia Mtingwa alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya
Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika
viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
No comments:
Post a Comment