Habari za Punde

Nani Atakaepata Tiketi ya Kuwakilisha Zanzibar Katika Michuano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika?

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi kuu soka ya Zanzibar mzunguko wa nne hatua ya 8 bora utaendelea Jumapili July 9, 2017 katika viwanja viwili tofauti, yani Amaan Unguja na Gombani Kisiwani Pemba.

Bingwa na Makamo Bingwa wa ligi hiyo watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mpaka ligi hiyo inakwenda mapumziko kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kila timu imecheza michezo mitatu ambapo  Jamhuri ndie kinara akiwa na alama 9 akipata ushindi michezo yote kwa asilimia 100, nafasi ya 2 inakamatwa na JKU yenye alama 6 huku Zimamoto ikiwepo nafasi ya 3 kwa alama 5 wakati Jang’ombe boys wapo nafasi ya 4 kwa points zao 4, wakati huo huo Okapi ikishika nafasi ya 5 na alama zao 4 ambapo Kizimbani wapo nafasi ya 6 kwa alama 3 huku Mwenge akiwa nafasi ya 7 kwa point yake 1 sawa sawa na Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya 8 kwa alama yao 1 .

Mzunguko wa 4 unatarajiwa kuanza Jumapili ya July 9, 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.