Habari za Punde

Waziri Mhe.Lukuvi Aifagilia Property International Maonesho ya Sabasaba.


Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, aifagilia Kampuni ya uuzaji, upimaji na ukopeshaji Viwanja ya Property International, baada ya kutembelea katika Banda lao la maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar esSalaam, leo mchana.
 Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kutembelea banda hilo, Lukuvi alisema kuwa Serikali haikufanya makosa waka kiini macho pale ilipotangaza kushusha bei ya tozo ya upimaji wa ardhi kwa asilimia 67 lengo ikiwa ni kila mwananchi awe katika makazi bora, kama ambavyo imekuwa ikifanya Kampuni hiyo kupima viwanja.
Aidha amesema tozo hizo zimeondolewa kuanzia Julai mosi hivyo taasisi za upimaji ardhi zitakazoendelea kuuza viwanja kwa gharama kubwa zitafutiwa vibali vya kufanya biashara hiyo. 
 Aidha Lukuvi alisema kuwa haitamvumilia mfanyabiashara yeyote asiyetekeleza agizo la serikali la kupunguza bei za upimaji kwakuwa mahitaji ya ardhi bora ya wananchi ni haki yao.
''Kuanzia Julai mosi tozo za gharama ya upimaji ardhi zimepunguzwa kwa asilimia 67 hivyo serikali inakusudia wananchi kuuziwa viwanja kwa bei nafuu.
 Waziri Lukuvi, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, baada ya kutembelea Banda hilo.
*********************************************
"Tunaposema tumekusudia kila mwananchi kujenga katika ardhi bora tunamaanisha hivyo na nyie wafanyabiashara mkubali mabadiliko hatukupunguza asilimia 67 kwa bahati mbaya,"alisema Lukuvi

Aliongeza kuwa"Uzeni viwanja kwa sura ya ubinadamu na nyie Property hakikisheni 
mnafuatilia maeneo yaliyotengwa ili kuwa katika mpango miji,"alisema. 
Alitaja maeneo hayo kuwa ni Mtwara Musoma na Iringa.
 Abdul Haleem, akizungumza na waandishi wa habari
*******************************************
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Property International, Abdulhaleem Zahran alisema kuwa amepokea na atayafanyia kazi maelekezo hayo ya Waziri na kumuahidi kuwa Kampuni hiyo itafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali ili kuweza kuwafikia wananchi wa chini.
Alisema ardhi isiyopimwa ina gharama kubwa hivyo kampuni hiyo itashusha gharama za viwanja kulingana na mahitaji yaliyopo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.