Habari za Punde

ZANTEL YAZINDUA ‘APP’ YA SIMU KUHAMASISHA UTALII WA NDANI NA KIGENI NCHINI.

· ‘App’ hii imelenga kuwasaidia watumiaji wake kupata taarifa muhimu kuhusu hoteli, usafiri, sehemu za vivutio, klabu, kasino, maduka makubwa, ubalozi na hospitali.
Dar es Salaam, Tanzania, Juni 29 2017. Kampuni ya simu za mkononi Zantel ambao wanaongoza katika utoaji wa huduma bora za data, leo imezindua application ya simu inayojulikana kama ‘Discover Tanzania Mobile App” ambayo lengo lake ni kuhimiza utalii wa ndani na nje kwa lengo la kuwapatia watalii taarifa sahihi za maeneo ya utalii yanayopatikana na hapa nchini Tanzania.
App hiyo itakuwa na taarifa zote za muhimu zinazopatikana hapa nchini zikiwamo kuhusu hoteli, usafiri, maeneo ya vivutio, kumbi za starehe, maduka makubwa, ubalozi na hospitali ambapo huduma hiyo itapatikana na kwenye Google Play Store kwa gharama nafuu ya Shilingi 500 tu.
Akizungumzia huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Zantel, Gasper Mbowa alisema, “Tunayofuraha kubwa kuzindua App hii ni kwa ajili ya wateja wetu, lakini jambo kubwa zaidi ni kuwa Zantel ndio Kampuni ya kwanza ya Mawasiliano kuanzisha huduma hii hapa nchini.”
‘Discover Tanzania mobile App’ ni rahisi kutumia na pia ni huduma ya bei nafuu kwa watu wote, kwa wageni na wenyeji. Kwa muda wa siku tatu mteja wa Zantel atatumia kiasi cha shilingi 500, kwa siku saba mteja atatozwa shilingi 2000 na kwa mwezi mzima mteja atatozwa 3,000. Aliongeza kuwa alama ya siri kwa ajili ya kupata huduma hiyo kupitia sms au sauti kwa wateja wa Zantel ni 15582 ambapo watatozwa Tsh. 1 tu kwa sekunde.
Alisema, hivi sasa nchini Tanzania taarifa zinahitajika zaidi kwa watalii ili kujua maeneo ya vivutio, aina za vyakula vinvyopatikana, maeneo ya burudani na gharama mbalimbali za huduma ikiwamo malazi, upatikanaji wa usafiri wa uhakika, maeneo yenye ofisi muhimu kama vile ubalozi, huduma za hospitali na kadhalika.
“Zantel sasa imekuwa ni sehemu ya kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kurahisisha shughuli za utalii. Ni imani yetu kubwa kwamba huduma hii itatangaza utalii kwa sababu taarifa zote muhimu zitakuwa zinapatikana kwa watalii wa ndani na wa nje ya nchi. Tutahakikisha tunahimiza usalama ili kuwawezesha watalii kuunganishwa moja kwa moja na huduma za Zantel,” alisema.
Aliongeza kuwa, application hiyo itapatikana kwenye simu zote za mfumo wa android pamoja na IOS kwa ajili ya simu aina ya I-Phones.
Sekta ya utalii nchini Tanzania ni eneo muhimu linalozalisha ajira takribani 250,000 kwa wananchi kila mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania inaingiza mapato yatokanayo na utalii yanayofikia Dola bilioni 2.

Kuhusu Zantel
Mtandao wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni miongoni mwa wawekezaji na wagunduzi kwenye sekta ya mawasilino wakiongoza kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja. Lakini zaidi ya yote, ni miongoni mwa kampuni ya mawasiliano inayokuwa kwa kasi kubwa na inayotengeneza faida kubwa katika Sekta ya mawasiliano Tanzania. Mtandao huu wa Mawasiliano Zanzibar ndiyo mtandao pekee wa huduma za mawasilino unaotoa huduma ya simu za nje kwa bei nafuu, simu na  bando kupitia mfumo bora wa CDMA, GSM na 3G.
Huduma za Zantel zimekuwa zikikua kutokana na kuongezeka watumiaji wake huku ikizidi kuonyesha ubora katika huduma zake ambazo kila mtu anaweza kuzimudu pamoja na kutoa huduma ya haraka ya mtandao wa wireles kwa haraka na ubora.
Zantel imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi kwenye sekta ya mawasiliano. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health.
 Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele kupata tarifa kwa haraka.
Kwa maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com

Kwa Mawasiliano zaidi:
Rukia Mtingwa

Website: www.zantel.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.