Habari za Punde

Bi.Rehema Juma Anaomba Msaada wa Kupatiwa Matibabu Kutokana na Uvimbe Unaomsumbua Kwa Miaka 17. Sasa Ili Apate Tiba.

Bi. Rehema Juma Kishena kama anavyoonekana pichani na uvimbe unaomsumbua kwa miaka 17 sasa.
Na Vero Ignatus, Arusha.
Mwanamke mmoja mkazi wa  Levolosi Arusha  bi Rehema Juma Kishena (40) anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka taktibani robo tatu ya uso wake .

Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua ,akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001  uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa  upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe
ulirudi tena kama awali.

‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.

Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa.

“Nawaombeni msaada ili niweze kujitibu kwani hali yangu kama mnavyoiona nipo kwa dada yangu hapa ,sina msaada wowote” alisema Bi. Rehema.

Kwa upande wake dada yake ( Rehema )Aziza Bakari Muyai amewaomba watanzania kushirikiana nae katika kumsaidia mdogo wake ili aweze kupatiwa matibabu kwani hali yake inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda.

Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373.
Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake wa ( 3) Sophia Dastan Mandia nyumbani kwa dada yake Levolosi mkoani Arusha. Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake Sophia Dastan Mandia pamoja na dada yake bi Aziza Bakari Muyai nyumbani kwake Levolosi Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.