Habari za Punde

Kete 560 za unga zakamatwa zikitokea Tanga

Na mwandishi wetu, Pemba
JUMLA ya kete 560 za unga zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya zimekamatwa na vikosi vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba zilizokuwa zikiingizwa kutoka Mkoa wa Tanga .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba , kamishna Msaidizi wa Polisi Haji Khamis Haji amesema kukamatwa na kete zimekamatwa zikiwa katika chombo chenye jina la SIYASEMI kikiwa na namba za usajili T 0058.
Amesema vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi kwa ushirikiano vilifanikiwa kukikamata chombo hicho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi ambao ni raia wema wakati kinajiandaa kuondoka katika bandari ya Tanga .
“Tumefanikiwa kukamata chombo chenye jina la SIYASEMI kikiwa na namba ya usajili T 0058 na baada ya kukipekua tulibaini kuwa kimebeba kete 560 za  unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroin” alieleza.
Aidha kamanda wa Haji amewataka wananchi kujitokeza kutoa ushirikiano na vyombo vya ulinzi ikiwa ni pamoja na kutoaa taafisa sahihi sambamba na kwenda kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani .
“Nawaomba sana wananchi waendelee kuviunga mkono harakati za vikosi vya ulinzi katika kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya kwa kuhakikisha wanatoa taarifa  sahihi sambamba na kutoa ushahidi wanapohitaji ”alisisitiza.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman ameviagiza vyombo vya ulinzi Mkoa huo kuimarisha doria sehemu za madiko ili kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya.
Aidha ameliagiza jeshi la Polisi kumkamata mahodha wa Chombo hicho ili aisaidie Serikali kuhakikisha mhusika na unga huo anapatikana na kufikishwa mahakamani .

“Anzeni na nahodha wa chombo hichi licha ya kwamba amesema hakuwemo kwenye safari  , mchukueni ili asaidie kumtambua mwenye mzigo huu kwani tumechoka kuona vijana wanaathirika na utumiaji wa dawa za kulevya ”alisema.

Kufuatia kufanikiwa kukamatwa unga huo , Mkuu wa Mkoa amevipongeza vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vimefanikisha kukamatwa kwa mzigo ambao , kama ungafanikiwa kuingizwa hapa nchini ungeleta athari kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.