Habari za Punde

Kongamano la Kimataifa la Nne la Diaspora Zanzibar Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar


Mwakilishi wa Kampuni ya TIC  Godfrey Mwambe akitowa Mada kuhusiana na Diaspora kuwekeza katika Jamii Nchini, akizungumza wakati wa Kongamano la Nne la Diaspora linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.   
Mwakilishi wa TPSF akizungumzia Mada kuhusiana na fursa kwa WanaDiaspora kuwekeza nyumbani akitowa mada hiyo kwa Watanzania Wanaoishi Nje kutumia fursa hiyo kuwekeza nyumba.
Baadhi wa WanaDiaspora wakifuatilia Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
Mtanzania anayeishi Nje Nchini Netherlands Dr. Eileen Petit Mshana akichangia wakati wa Kongamano hilo lililofanyanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff Zanzibar akichangia mada.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo Dk Hikman na Watoa Mada wakifuatilia Michango iliokuwa ikuwasilishwa wakati wa Kongamano hilo la 4 la Watanzania Wanaoishi Nje Diaspora lililoandaliwa na Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
Mkurugenzi Huduma za PBZ Islamic Said Mohammed Said akitowa Mada kuhusiana na utoaji wa huduma za kibenki kupitia Benki ya Watu wa Wazanzibar  PBZ, kwa Watanzania wanaoishi Nje Diaspora wakati wa Kongamano hilo la 4 la Kimataifa lililofanyika Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kikao cha Kongamano Mhe Hassan Khamis Hafidh akiongoza kikao hicho kikizungumzia Mada ya Diaspora and Country Development Masda zilizowakilisha na Dr Haroub Maalim kulia kutoka SUZA na Mwakilishi wa Taasisi ya Milele Fuondation Eshe Ramadhani wakiwa katika meza kuu. wakifuatilia.  
Dr. Haroun Maalim akizungumzia Mada kuhusiana na programm ya Kiswahili inayotolewa na Chuo Kikuu cha Suza wakati wa Kongamano hilo la Watanzania wanaoishi Nje Diaspora lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar SUZA inatowa elimu ya Juu katika somo la kiswahili na kuwataka watamzania wanaoishi nje kuja kutowa Elimi hiyo kwa Wanafunzi wanaojiunga katika Chuo hicho kupata elimu ya Kiswahili Zanzibar.
Mwakilishi wa Milele Foundation Eshe Ramadhani akielezea Mada kuhusiana na Taasisi yao inayotowa huduma za kijamii kwa Wananchi katika sekta ya kijamii za Afya Elimu na nyeginezo kupitia Diaspora.
Mwanadiaspora Haji Rajab Haji akichangia mada wakati wa Kongamano hilo la Watanzania wanaoishi Nje Diaspora wakati wa kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa hoteli yac sea cliff Zanzibar. 
Mshiriki wa Kongamano la 4 la Diaspora Said akichangia Mada wakati wa hafla hiyo ya Kongamano la 4 la Diaspora Zanzibar. 


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Salum Maulid Salum akijibu michango iliowasilishwa wakati wa Kongamano hilo hatua uliochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushughulikia michango inayotolewa na WanaDiaspora katika Nchi yao na kuwatambua. 
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Tanzania Balozi Anisa Mbega akitowa ufafanuzi wa Michango iliowasilishwa na WanaDiaspora wakati wa Kongamano hilo la 4 la Kimataifa lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.