Habari za Punde

Matembezi ya Baraza la vijana kuadhimisha mwaka mmoja wilaya ya mjiniMkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud akiwa Sambamba na Mkuu wa wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Thomas mara baada ya kupokea matembezi yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini katika kusheherekea kutimiza mwaka mmoja pamoja na kuelekea maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "VIJANA NI WAJENZI WA AMANI". 

Matembezi hayo yalianzia Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya mjini mpaka Mapinduzi Square hapo Kisonge ambapo palifuatiwa na zoezi la uchangiaji damu. 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi pamoja na Mkuu wa wilaya ya mjini pia walishiriki matembezi hayo katika kuwaunga mkono vijana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.