Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya Mwenge na Taifa ya Jangombe Mchezo Unaofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Taifa ya Jangombe Imeshinda Bao 3--1.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Khamis Faki akimpita beki wa Timu ya Mwenge Said Mbarouk wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan.Katika mchezo huo Timu ya Jangombe inaongoza kwa mabao 3-1. 
 Timu ya Mwenge imeandika bao lake la kwanza kupitia mshambuliaji wake Ali Hassan katika dakika ya tatu ya mchezo huo kipindi cha kwanza bao la Taifa ya Jangombe la kusawazisha limefungwa katika dakika ya 45 ya mchezo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Mohammed Salum. hadi mapumziko timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili kiliaza kwa timu ya Taifa ya Jangiombe kulishambulia lango la Mwenge katika dakika ya 51 imeandika bao la pili lililofungwa na Adam Ibrahim. Timu ya Taifa ya Jangombe imeandika bao lake la tatu kupitia mshambuliaji wake Ali Badru.       
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Mohammed Salum akimiliki mpira huku beki wa Timu Mwenge Said Mbarouk akijirabu kumzuiya wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda 3--1
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Mohammed Salum na mchezaji wa Timu ya Mwenge Said Mbarouk wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.


Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Khamis Faki akimpita beki wa Timu ya Mwenge Said Mbarouk, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda bao 3--1 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.