Habari za Punde

Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya

Na Salmin Juma, Pemba

Jumla ya watuhumiwa  6 wa madawa ya kulevya mkoa wa kusini Pemba  wametiwa hatiani na jeshi la Polisi kwa uuzaji na ungizaji  wa dawa hizo.

Akizungumza na redio Istiqama  kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, Mh, Mohd Sheikhan Mohd amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Tanausu Gomeza Canu raia wa Hispania, Fabrizio Ravalt raia wa Italy, Saburi Ali Hamad mkaazi wa Msingini, Ramadhan Said Mohd mkaazi wa Chachani,Faki Khamis Ali Mkaazi wa Msingini, na Hamad Juma Hamad mkaazi wa Mtoni.

Sheikhan amesema watuhumiwa wote hao walipandishwa mahakamani na hadi kufikia sasa tayari wameshapatiwa hukumu  kwa mujibu wa makosa yao.

Kamanda huyo amesema  mkoa wake umekuwa na sifa mbovu ya madawa ya kulevya hivyo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha wanawakamata wale wote wanaojihusisha na madawa hayo ambayo yanapelekea kuathiri wimbi kubwa la vijana na kupelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Sheikhan ameyataja baadhi ya maeneo ya mkoa wa kusini Pemba ambayo yameathirika zaidi na dawa hizo ni pamoja na  Machomane, Michakaini, Ndugu kitu, Msingini ,Miembeni, Muambe, Kengeja na Mkoani na kuwataka masheha na wazee wa vijiji kushirikiana na jeshi la polisi  kwa kulipatia taarifa kwani  wananchi wakishiriki kikamilifu  hakuna kinachoharibika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.