Habari za Punde

NEGRO DAY KESHO, WATAKIPIGA NA TAIFA YA JANG’OMBE AMAN USIKU

Na: Abubakar Khatib Kisandu, 
Tamasha la Negro Day litafanyika kesho Jumanne Agost 29, 2017 ambapo timu ya Negro FC itacheza mchezo maalum wa kirafiki na Timu ya Taifa ya Jang’ombe mchezo ambao utasukumwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa Negro FC Hussein Ahmada amesema katika Tamasha hilo wao Negro watalitumia pia kwaaajili ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya ambao wamesajiliwa kwaajili ya msimu mpya wa mwaka 2017-2018.

Amesema pia watatangaza Benchi jipya la ufundi wakiwemo kocha mkuu na msaidizi wake pamoja na kumtangaza mfadhili wao mpya ambae ni mkorea.

Aidha Ahmada amesema watazitambulisha jezi zao mpya na pia kutakuwa na burudani mbali mbali katika Tamasha hilo ambalo litaadhimishwa kila mwaka siku ya Agost 29.

“Negro day ni siku maalum kwetu kwa kila mwaka ikifika Agost 29 tutafanya tamasha maalum, tutawatangaza wachezaji wetu wapya, benchi la ufundi pamoja na mfadhili wetu tutamtangaza na mambo mengine mengi tu”. Alisema Ahmada.

Negro FC inashiriki ligi daraja la Pili Taifa Unguja.
Attachments area

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.