Habari za Punde

Chama cha Mpira wa Kikapu Wilaya ya Mjini Waanda Mashindano Makubwa Yatakayodhaminiwa na Kampuni ya Kutoka Marekani.


Na: Abubakar Khatib Kisandu, 
Chama cha Basketball Wilaya ya Mjini (UBA) kinatarajia kuanzisha mashindano ya Mpira wa Kikapu kwa Wanaume yananayotarajia kuanza rasmi Septemba 9, 2017 katika viwanja vya Gymkhana Mjini Unguja na katika ufunguzi huo siku hiyo kutapigwa mchezo kati ya timu ya POLISI dhidi ya MBUYUNI.

Katibu wa Basketball wilaya ya mjini Saidi Ali Mansabu amesema mashindano hayo wamepata wadhamini kutoka kiwanda cha kutengeneza Jezi cha UTA ambacho kipo Marekani.

“Mashindano yetu tunatarajia kuanza Septemba 9, 2017 ambapo tumepata wadhamini kampuni moja ya kutengeneza Jezi inaitwa UTA ipo Marekani, wametudhamini Jezi na mahitaji mengine katika Mashindano haya, nawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kwasababu haya ni mashindano makubwa sana kwa vile wadhamini ni wenye mpira huu”. Alisema Mansabu.

Jumla ya timu 14 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo ambayo yataanzia kwa hatua ya makundi kwa kupangwa makundi mawili, kundi A na kundi B ambapo timu nne za juu kwa kila kundi zitatinga hatua ya robo fainali kisha moja kwa moja kupatikana timu nne za nusu fainali kisha kucheza timu mbili kucheza fainali.

Miongoni mwa timu zilizothibitisha kushiriki ni Polisi, Mbuyuni, Stone Town, Africa Magic, Betras, Zan Kwerekwe, Ranger, New West na Nyuki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.