Habari za Punde

Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Afungua Mkutano wa Kamati ya Kuzungumzia Kukabiliana na Wanafunzi na Wachumaji Karafuu Pemba.

AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, Ali Salum Matta akifungu kikao cha kamati ya Kujadili, kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa wanafunzi na wachumaji wa karafuu walioko katika kambi, kikao hicho kimefanyika mjini chake chake.
MRATIB wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Pemba, Khamis Arazak Khamis, akitoa ufafanuzi juu ya maandalizi ya kamisheni ya kukabiliana na maafa Pemba zilivyojiandaa pindi ikitokea maafa katika kambi za wachumaji wa karafuu Pemba.
AFISA mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Bakari Ali Bakari akielezea mikakati yake juu ya kukabiliana na maradhi ya Mripuko pindi yatakapotokea
MWAKILISHI wa Wizara ya Afya Pemba, Msanifu Othman Massoud, akitoa tathmini ya maradhi ya mripuko yaliyotokea katika kipindi cha Aprili hadi Julai mwaka huu, katika kikao cha kujadili, kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa wanafunzi na wachumaji wa karafuu walioko katika kambi
AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Salum Kitwana Sururu, akitoa ufafanuzi juu ya kambi za wanafunzi zinazotarajiwa kuanza muda wowote Kisiwani Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.