RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akizungumza na waalimu, wanafunzi,
wazazi na wananchi wengine kwenye tamasha la 53 la elimu bila ya malipo,
lililofikia kilele chake jana uwanja wa Gombani Chakechake kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyeki wa
Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, ametangaaza kufuta michango ya
elimu ya sekondari, kwa skuli za serikali kuanzia mwezi Julai mwaka 2018, na
kuitaka wizara ya fedha kuiangalia upya bajeti kuu ya Wizara ya elimu Zanzibar.
Alisema
uwezo huo serikali unao, bila ya kuomba ufadhili kutoka kwa wafadhili wa nje ya
nchi, kama ilivyofanya kwa kufuta michango kama hiyo kwa elimu ya msingi, hivyo
nayo ya sekondari itafutwa kuanzia mwakani.
Dk
Shein, ameeleza hayo uwanja wa wa michezo Gombani Chakechake kisiwani Pemba, wakati
alipokuwa akizungumza na mamia ya wanafunzi, wazazi, wananchi na watendaji
wengine wa serikali, kwenye kilele cha
maadhimisho ya miaka ya 53 ya Elimu bila ya malipo yaliofanyika kisiwani Pemba
kitaifa.
Alisema
kwa vile muasisi wa taifa hili, alitangaaza elimu bila ya malipo miaka 53
iliopita, sasa lazima na serikali anayoiongoza itekeleze hilo kwa vitendo, ndio
maana alianza kwa elimu ya msingi na sasa kuanzia mwakani, ni kwa elimu ya
sekondari.
Alisema
anaamini bejti kuu ya wizara ya elimu, inatosha kugharamia elimu ya sekondari,
na ndio maana akaiagiza wizara ya fedha kuiangalia tena upya bajeti ya wizara
ya elimu ya mwaka wa fedha 2018/2019.
“Na
michango ya elimu ngazi ya sekondari nayo natangaaza kuifuta kuanzia tarehe
1/7/2018, kama nilivyofuta michango ya elimu ya msingi kwa skuli zote za
serikali”,alisema.
Akizungumzia
kuhusu ubora wa elimu, Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, alisema serikali inaendelea kuimarisha pia
majengo kwa kuzifanyia matengenezo na upanuzi wake.
Alisema,
serikali inampango wa kujenga skuli tisa za ghorofa kwa Unguja na Pemba, skuli 23
kufanyiwa upanuzi na kuongezwa vyumba vyengine vya madarasa, kuweka samani,
ujenzi wa maabara ya sayansi na ununuzi wa vitabu.
Alifafanua
kuwa, aidha jengine katika kuimarisha sekta ya
elimu, serikali itaendelea
kukabiliana na changamoto nyengine mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kuimarisha
maslahi ya waalimu kwa kulipa malimbikizo yao mbali mbali.
Hivyo,
ameiagiza wizara ya elimu, kuhakikisha wanalifuatilia hilo kwa haraka, ili
waalimu wafanye kazi zao kwa ufanisi kama walivyowafanyakazi wengine wa sekta
ya umma.
“Naamini,
niliongeza mshahara ya watumishi wa umma kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi
300,000 ambapo naamini na waalimu wakiwa kama watumishi wa umma, nao
wamefaidika na hilo”,alifafanua.
Aidha
amewataka waalimu hao kuendelea kufanya kazi zao kwa kufuata maadili, kanuni na
sheria za utumishi za uuma, ili watoe elimu kwa ufanisi wawapo madarasani.
Alisema
waalimu ndio kioo cha jamii, hivyo lazima hilo walielewe kwa kufanyaka kazi zao
vyema, ili wazalishe wanafunzi bora waliojaa elimu.
Katika
hatua nyengine, Rais huyo wa Zanzibar, amewataka wazazi na walezi, kuendelea
kufuatilia nyenendo za watoto wao, ili kuhakikisha wanafika madarasani.
Alisema
wazazi hao wanaomchango mkubwa, katika kufanikisha ubora wa elimu nchini, kwa
kule kuwaharakisha watoto wao, kwenda skuli sambamba na kuwataka wadurusu
masomo yao.
“Wazazi
na nyinyi lazima tuungane pamoja na waalimu, katika kufuatilia nyenendo za
watoto wenu, kwa kuwakumbusha kudurusu masomo na lazima muhakikishe wanafika
masomoni kwao”,alifafanua.
Mapema
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe: Riziki Pembe Juma, alisema
sherehe hizo za elimu bila ya malipo zilizoamshwa na Rais wa Zanzibar,
zimerejesha umoja na mshikamano miongoni mwa waalimu, wanafunzi na watendaji wa
wizara yake.
Alisema
sherehe hizo ambazo miaka ya 2000 zilionekana kusuasua, na sasa kuibuliwa upya
kwa mawazo ya rais wa Zanzibar, yameirejeshea heshima wizara ya elimu kwa
kuendelea kuibua vipaji vya kimichezo.
Mapema
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Khadija Bakar Juma alimpongeza rais huyo wa
Zanzibar kwa kufuta michango ya elimu kwa wanafunzi wa skuli za serikali.
Hata
hivyo, Katibu Mkuu huyo aliwataka wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wao
skuli ya msingi, kwani hakuna michango yoyote skulini hapo baada ya kufutwa na
rais wa Zanzibar.
Awali
rais huyo wa Zanzibar alipokea maandamano ya wanafunzi wa mikoa mitano ya Zanzibar, yalioanzia nje ya uwanja
wa Gombani, na kisha kukabidhi zawadi kwa washindi wa michezo, huku mshindi wa
jumla ukiwa ni Mkoa wa kusini Pemba ambapo walikadhiwa kikombe na Rais wa
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment