Habari za Punde

Ukumbi wa Mpya wa Burudani na Muziki wa Kisasa Kuzinduliwa Jijini Mwanza.

Na Binagi Media Group
Klabu mpya ya muziki yenye hadhi inayokubalika kwa viwango vyote vya kitaifa na kimataifa inatarajiwa kuzinduliwa Jijini Mwanza, ikilenga kukata kiu kwa wapenzi wa burudani ndani na nje ya Tanzania.

Klabu hiyo inajulikana kwa jina la “CLUB 55” na inapatikana jengo la Delux Hotel katikati ya Jiji la Mwanza ilipokuwa zamani klabu iliyokuwa ikiongoza kwa burudani Afrika Mashariki ya Delux Club.

Meneja Msaidizi wa CLUB 55, Nickson Bubelwa Kyaruzi amesema uzinduzi wa klabu hiyo utafanyika kesho Septemba 14,2017 kuanzia majira ya saa tatu kamili usiku kwa wageni waalikwa na burudani ya kukata na mundu itafunguliwa kwa watu wote ijumaa Septemba 15,2017 kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi tu.

Meneja wa Klabu hiyo, Ben Mwangi amesema imeboresha kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwa klabu nambari moja kwa ubora na burudani Jijini Mwanza, kuanzia huduma kutoka kwa wahudumu waliofunzwa vyema, usalama wa bidhaa pamoja na wateja kuanzia ndani na nje ya ukumbi wa klabu hiyo.

Meneja wa Club 55, Ben Mwangi (kulia) akizungumzia uzinduzi huo. Kushoto ni Meneja Msaidizi Nickson Kyaruzi 
Matukio yakiendelea kuchukuliwa ndani ya CLUB 55 Jijini Mwanza
Wanahabari kazini
Meneja wa Club 55, Ben Mwangi akionyesha mtambo wa kutibu maji kabla ya kugandisha barafu katika klabu hiyo
Meneja wa Club 55, Ben Mwangi akionyesha barafu zilizogandishwa klabuni hapo
Glasi zilizosafishwa vyema kwa maji ya moto klabuni hapo
Miongoni mwa kaunta klabuni hapo
Club 55 Jijini Mwanza
Usikose Ijumaa Septemba 15,2017 kuanzia saa tatu kamili hadi kuchee ndani ya Club 55 (zamani Delux Hotel) Jijini Mwanza kwa mtonyo wa buku kumi tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.