Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Simba Kikijifua Katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Kujiandaa na Mchezo Wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kocha Msaidizi wa Timu ya Simba akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi yao katika uwanja wa Amaan Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Watani wao Timu ya Yanga African mchezo unaotarajiwa kufanyika jumamosi Jijini Dar es Salaam. Kikosi cha Timu ya Simba kimewasili jana Zanzibar kwa boti ya Azam Marine ya Kilimanjaro V kuweka kambi yake Visiwani Zanzibar.
Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Joseph Omog akifuatilia mazoezi hayo katika uwanja wa Amaan Zanzibar akiwa na Meneja wa Timu na Daktari. wakiwa katika uwanjani.
Kikosi cha Timu ya Simba wakiwa katika mazoezi yao katika Uwanja wa Amaan Zanzibar leo asubuhi wakijinowa kwa mchezo wao na Timu ya Yanga African.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.