Na.Haji Nassor - Pemba.
LIGI kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba,
inatarajiwa kuendelea tena leo, kwenye viwanja viwili tofauti, ambapo kwenye
uwanja wa FFU Finya, Okapi yenye point nne, wakiwaalika Opec yenye point mbili.
Katika
uwanja wa Gombani, wenyeji wa uwanja huo, timu ya Younger Islanders yenye
pointi sita, ikishika nafasi ya pili, itawakarabisha Hard rock ambayo ina point
mbili, tayari timu zote zimeshashuka uwanjani mara tatu.
Kesho ni
zamu ya wakongwe wa soka wa Jamhuri, yenye point nne, ikishika nafasi ya tatu, watakaoumana na
Chuo basra yenye point mbili, mchezo unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa FFU Finya majira
ya saa 10:00 jioni.
Kesho hiyo
pia, ndani ya dimba la Gombani New star yenye point nne, itawakuwa wageni wa
FSC yenye pointi sita, baada ya kushinda michezo miwili na kufungwa mmoja.
Wakati ligi
kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, ikitoka kwenye mapunziko mafupi, baada ya
kuendelea tena leo, timu ya Mwenge ndio vinara wa ligi hiyo, ikijikusanyia point
tisa, wakati Islanders, FSC na Shaba wakikabana koo kwenye nafasi ya pili kwa
point sita.
Timu
zinazoshindana kukokota mkia wa ligi kuu Zanzibar kituo cha Pemba, ni pamoja na
Wawi star yenye point moja, Opec, Dodo moro, Chuo basra na Hard rock zikivutana
kwa kuwa na pointi mbili mbili, baada ya kucheza michezo mitatu.
No comments:
Post a Comment