Habari za Punde

Mawaziri wasio na Wizara maalum watembelea kambi za karafuu kisiwani Pemba

 Mmiiliki wa kambi ya Karafuu ilioko kwa Changawe Mkoani Pemba, Haji Ali Haji, kutoka mkaazi wa Kiuyu Penjewani, akielezea kwa masikitiko juu ya kuvamiwa na kuibiwa Karafuu zake ndani ya Kambi hiyo na watu wasiojuilikana .

 Karafuu ambazo hazajiaanikwa kutokana na upungufu wa majamvi , ingawaje mmiliki wake alitakiwa kwenda ZSTC kukopeshwa lakini bado analilia gharama kubwa .

Moja ya mkarafuu ambao hadi sasa , hazijafikia hatuwa ya kuchumwa kwa vile hazija komaa kwa ajili hiyo huko Changaweni Mkoani Pemba.
Waziri asiekuwa na Wizara maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Juma Ali Khatib, akielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinazochukuliwa na kamati za Ulinzi na usalama za Wilaya na Mkoa katika uokoaji wa zao hilo ambalo ndani ya Wilaya ya mkoani kumekuwa na mafaniko makubwa baada ya kuangalia uchumaji wa karafuu hizo huko katika eneo la Wambaa wakati ya ziara yao ya kuangalia maendeleo hayo
 Waziri asiekuwa na Wizara maalumu, wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Said Soud Said, akizungumza na wamiliki wa kambi ya karafuu ya Kwa changawe Mkoani na viongozi mbali mbali wa Serikali na kupata fursa ya
kuwafariji Wamiliki hao baada ya kuibiwa Karafuu zao kavu zenye thamani ya Tshs, 800, 000/= katika kambi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, akitowa maelezo mbele ya Waziri asiekuwa na Wizara maalumu , Juma Ali Khatibu , wakati alipokuwa na Ziara ya kutembelea Kmabi za Karafuu kuona
maendeleo ya uokoaji wa zao hilo huko katika eneo la kwa Changawe Mkoani Pemba.
.


PICHA NA BAKAR MUSSA -PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.