Habari za Punde

Uzinduzi wa uwekaji lami bara bara ya Kilo mita 35 ya Ole - Kengeja

 Gari ya Wizara ya miundombinu, Mawasiliano  na Usafirishaji Pemba, ikimwaga Lami ya kwanza  (Primo) kwa ajili ya uzinduzi wa uwekaji lami bara bara ya Kilo mita 35 ya Ole Kengeja huko katika eneo la OleKianga.
 Ofisa mdhamini Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Baucha , akiangalia gari hilo linavyomwaga Lami hiyo huko katika bara bara ya Ole -Kengeja Pemba.


Ofisa Mdhamini Wizara ya Miundombinu , Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Baucha, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa uwekaji wa Lami katika bara bara ya Ole -Kengeja , baada ya kufanya uzinduzi huo kwa kuweka Lami ya mwanzo ( Prima)
 Wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu , Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, wakifanya usafi katika bara bara ya Ole -Kengeja , kabla ya kufanyika uzinduzi wa kuweka Lami ya Prima, katika Bara bara hiyo huko katika eneo la Ole- Kianga.
Akinamama wa Shehia ya ya Ole na Uwandani Pemba, wakisafisha bara bara ya Ole - Kengeja , baada ya kupatiwa ajira za muda kabla ya kuwekewa Lami ya PRIMA 

PICHA  NA BAKAR MUSSA-PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.