Habari za Punde

Dk Shein amtumia salamu za pongezi Sultan Qaboos wa Oman


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Sultan wa Oman,Qaboos Bin Said Al Said pamoja na wananchi wa nchi hiyo kwa kuadhimisha Siku ya Taifa hilo.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Oman katika kusherehekea siku hii adhimu kwa Taifa hilo.

Aidha,katika salamu hizo,Dk.Shein alimuhakikishia Sultan Qaboos Bin Said Al Said kuwa 
Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Oman sambamba na kuimarisha udugu uliopo kati ya wananchi wa Oman na wananchi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo, salamu salamu hizo zilieleza kuwa siku hii adhimu inaendelea kutoa nafasi zaidi ya mashirikiano kati ya pande mbili hizo pamoja na kupongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Oman katika kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo.

Dk.Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Oman 
afya njema na sherehe njema katika kuadhimisha siku hiyo huku akimtakia kiongozi huyo
mafanikio zaidi katika kuendelea kuipatia maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo
kwa madhumuni ya kulinufaisha Taifa hilo patoja na wananchi wake.

Oman ilipata Uluru wake kutoka ukoloni wa Kireno mnamo Novemba 18 mwaka 1650
chini ya kiongozi na muasisi wa Taifa hilo Imam Sultan Bin Saif Bin Malik Al Yarubi
ambaye alisimamia kung'oka kwa koloni hilo kutoka Oman pamoja na bandari 
zote za nchi hiyo zilikuwa chini ya Ureno.

Rajab Mkasaba,Ikulu Zanzibar.     0777427449

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.