Habari za Punde

Kozi ya Makocha ZFA Wilaya ya Magharibi B Unguja Yafungwa.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kozi ya makocha wa Mpira wa Miguu ngazi ya awali imefungwa leo Ijumaaa Novemba 3, 2017 saa 3.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa ZFA Wilaya Magharibi B uliopo Mwanakwerekwe Ijitimai.

Katibu Mkuu wa ZFA Wilaya ya Magaharibi B Omar Abuu amewataka makocha 
29 waliyomaliza kozi hiyo kufundisha soka kwa uzalendo na si kuvikomo vilabu kwani mafanikio ya makocha hayaji kwa haraka.

Awali, Mkufunzi wa kozi hiyo anaetambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Nassra Juma amewapongeza Makocha hao huku akiwashukuru pia ZFA kwa kuandaa kozi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.