Habari za Punde

Mawaziri Wanne Kutoka Nchini Ungada Watembelea Geita Kujifunza Uchimbaji Mdogo wa Madini Tanzania.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa miwani na Koti la kijivu akimpokea Waziri wa Madini wa Uganda Mheshimiwa  Lokeris Peter  baada Mkoani Geita na ujembe wa Mawaziri wanne na wanasheria kwa ajili ya kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyowawezesha wachimbaji wadogo, Kati na Wakubwa katika Shughuli zao.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo Mwenye kizibao cha rangi nyukundu akiwa na viongozi wa Mkoa wa Geita pamoja na Mawaziri wanne wa Serikali ya Uganda baada ya Kuwasili Mkoani Geita kujifunza uchimbaji mdogo, Kati na Mkubwa wa Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wa kwanza kulia akiwaongoza Mawaziri kutoka Uganda kwenda kukagua shughuli za uchimbaji mdogo Lwamgasa Wilayani Geita.
Mawaziri wanne kutoka kutoka Uganda pamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita wakujionea shughuli za ujenzi wa Kituo cha mfano cha Serikali zinavyoendelea katika eneo la Lwangasa Wilayani Geita. Kituo hiki kinajengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo akiongozana na Mawaziri kutoka Uganda pamoja na wataalamu wa Madini kukagua shughuli za uchimbaji mdogo wa madini katika mgodi wa Kadeo Lwamgasa Geita.

Mmiliki wa Mgodi wa KADEO Mine Limited ndugu Kadeo akitoa maelezo kwa Mawaziri na wataalmu wa madini walipotembelea Mgodi wa KADEO Mine kujifunza shughuli za uchimbaji mdogo wa Dhahabu Kata ya Lwamgasa Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita mwenye koti la kijivu na miwani akiwaongoza Mawaziri  kutoka Uganda kukagua shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa KADEO.
PICHA ZOTE NA Magesa Jumapili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.