Habari za Punde

Mchezo wa Kirafiki wa Timu ya Zanzibar Heroes na Taifa ya Jangombe Uwanja wa Amaan Timu Hizo Zimetoka Sare Bao 1 - 1.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kilichotoka sare na Timu ya Taifa ya Jangombe katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Kenya mwezi ujao.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Jangombe Wakombozi wa Ngambu kilichotoka sare na Timu ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana usiku uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mchezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1 - 1.
Kipa wa Timu ya Zanzibar Heroes akiondoa mpira huku mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe akiwa katika harakati za kutafuta bao.
Wapenzi wa Mpira wa miguu Zanzibar wakifuatilia mchezo wa kirafiki wa Timu ya Zanzibar Heroes katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.