Habari za Punde

Mhe. Eng Masauni Afungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akipiga makofi baada ya kuwasili  katika Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho,mkoa wa Dar es Salaam, Mkutano huo umefanyika leo Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam
Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti anayemaliza muda wake   wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha,   akizungumza wakati wa   Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto  aliyevaa kofia ni Mgeni Rasmi na Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni. Mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam
Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha Uongozi , Kiongozi anayemaliza muda wake katika Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Ibrahim Mpwapwa (kulia), wakati wa mkutano uliofanyika leo,ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.