Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Muungano Mchezo wa Netiboli Kati ya JKU na KVZ Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Gymkhana Zanzibar Timu ya KVZ Imeshinda Kwa Mabao 47 - 45.

Mchezaji wa Timu ya KVZ Agnes Ayoub (GS) akidaka mpira huku mchezaji wa Timu ya JKU Magori Khamis (GK) akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Kombe la Muungano michezo inayofanyika katika Viwanja vya Gymkhana Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa mabao 47 - 45.

Michuano hiyo inayofanyika katika viwanja vya Gymkhana michezo huaza saa mbili asumbu matokeo ya leo katika michezo mitano iliyochezwa katika uwanja huo ilishirikisha Timu kumi, mchezo wa kwanza ulizikutanisha Timu za Polisi Arusha 37 na Polisi Morogoro imeshinda mchezo huo kwa mabao 40, mchezo wa Pili umezikutanisha Timu za Jeshi Stars 47 na Timu ya Duma imepata mabao 27, mchezo wa Tatu umezikutanisha Timu za Zimamoto 29 na Bibinwa Watetezi Timu ya Uhamiaji imeshinda kwa mabao 61, Mchezo wa Nne umezikutanisha Timu za Afya 28 na Polisi Morogoro  imeshinda mchezo huo kwa mabao 49 na mchezo wa mwisho uliokuwa Kati ya JKU 45 na KVZ.47   No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.