Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe Eng.Masauni Atembelea Mradi wa Ujenzi Nyumba Mpya za Askari Poilisi Mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na  familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari hao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara, Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, baada ya  kukagua nyumba za  askari polisi na  familia zao zilizopo  kata ya Mukonde, Mkoani Mara,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, akitoa ufafanuzi juu ya  mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na  familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara kwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari
Familia za askari wanaotarajiwa kuhamia katika nyumba mpya zilizopo katika eneo la Mukonde, wakimsikiliza Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.