Na. Gabriel Ng’honoli
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
Takribani raia 800
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekimbilia Nchini Tanzania kuomba
hifadhi ya ukimbizi katika kijiji cha Kigadye Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma
wakihofia machafuko.
Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu
kusini mwa Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na
vikundi mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu
na hivyo kuanza kukimbia nchini Tanzania
kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Wakizungumza mbele ya
kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyotembelea katika kituo cha
kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia hao walisema sababu
iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa maisha yao kutokana na
mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na Serikali iliyopo
madarakani.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mst.) Emannuel Maganga akiongoza kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika kuwaona raia hao na wanafana
jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma muimu za kibinadamu zinaboresha
katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa
kuwasikiiza raia hao.
Kutokakana na wimbi
kubwa hilo huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi zinahitajika haraka ili
kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na watoto.
Baadhi ya raia
waliokimbilia nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na kuahirishwa Uchaguzi Mkuu
uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka kwa mzozo wa mapigano uenda
ukawaathiri amani nchini Congowa, Vyama
vya upinzanu vimeanza kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi,
wamehofia amani.
Kituo cha kigadye
wilayani kasulu, huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia wa Congo
wanaoendelea kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini mwao. Kusini
mwa Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio ya mara kwa mara
yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.
Habari na Picha zimeandaliwa na.
Gabriel
Ng’honoli
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
No comments:
Post a Comment