Habari za Punde

ZANZIBAR HEROES UTAIPENDA TU, YASHINDA 5-2Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) leo kwa mara ya kwanza mwaka huu imefanikiwa kupata ushindi baada ya kuifunga Villa United (Mpira Pesa) mabao 5-2, kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa saa10 jioni katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Heroes yamefungwa na Salum Songoro dakika ya 26, 66, Hamad Mshamata dakika ya 67, Amour Suleiman "Pwina" dakika ya 68 na Kassim Suleiman dakika ya 69 huku mabao yakufutia machozi ya Villa yamefungwa na Abdul swamad "Brown" dakika ya 26 na Mohd Mussa dakika ya 41.

Huu ni mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Heroes kufuatia awali kutoka sare ya bao 1-1 na Kombain ya Unguja, kisha wakatoka tena sare kama hiyo na Taifa ya Jang'ombe.

Heroes wataendelea tena kucheza michezo ya kirafiki ambapo watacheza na timu ya Dulla Boys siku ya Jumamosi saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Jambiani kisha watamaliza mchezo wa mwisho siku ya Jumapili na Kombain ya Makocha mchezo utakaopigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.