Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi Kati ya Jamuhuri na Mwenge Uwanja wa Amaan Zanzibar Mwenge Ikiongoza Kwa Bao 1-0.

 Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri Mussa Ali akimpita beki wa Timu ya Mwnge wakati wa mchezo wao wa ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotimua vumbi leo katika uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Jamuhuri ikingoza mchezo huo kwa bao 1 -0, lilifungwa na mshambuliaji wa Timu ya Mwenge katika dakika ya 31 kupindi cha kwanza cha mchezo huo. 
Mchezo wa saa 8, mchana ulizikutanisha Timu za Mlandege na JKU, Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa mabao 2 - 1 Mabao ya mlandege yamefungwa bao la kwanza la mlandege limefungwa na Khamis Abuu katika dakika ya 18 ya mchezi kipindi cha kwanza. bao la Pili la Mlandege limefungwa na Abubakar Ame katika dakika ya 60 ya mchezo kipindi cha pili bao la JKU limefungwa na Khamis Abdallah katika dakika ya 34 kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Timu ya Mwenge kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Kikosi cha Timu ya Jamuhuri kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri kushoto Mussa Ali na beki wa Timu ya Mwenge Haysam Khamis kulia wakiwania mpira wakati wa mchezo waufunguzi wa Kombe la Mapinduzi linalofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mwenge ikiongoza kwa Bao 1-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri akijaribu kumpita beki wa Timu ya Mwenge Yussuf Said wakati wa mchezo wao wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo unaofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya Mwenge ikiongoza kwa bao 1-0.
Beki wa Timu ya Mwenge Haysma Khamis kushoto na mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri Mussa Ali wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi mchezo unaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Mwenge ikiongoza kwa bao 1 -0.

Kocha Mkuu wa Timu ya Mwenge Salum Bausi akitowa maelekezo kwa timu yake kabla ya kuaza kwa mchezo wake na Timu ya Jamuhuri katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mwenge imeshinda bao 1 -0.

Imetayarishwa na OthmanMapara
Zanzinews.com.
Email.othmanmaulid@gmail.com.. 
0777424152
0715424152.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.