Habari za Punde

                           SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO

 Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223               7313                                                                                     Idara ya Habari Maelezo
Fax: 0255 24 2237314                                                                                                                     P.O. Box 2754
E-mail:habarimaelezo@yahoo.co.uk, maelezozanzibar@zanlink.com                             Zanzibar             
maelezozanzibar@hotmail.commaelezozanzibar@gmail.com                                                    
 
                          
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
(TANZIA)
 Kesho saa 6:00 mchana mwili wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Marehemu SGT Issa Saleh Issa aliyekuwa majeruhi akipatiwa matibabu nchini Uganda baada ya shambulio la Waaasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal I.

Marehemu SGT Issa Saleh Issa alikuwa katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Baada ya kuwasili kwa maiti hiyo, itapelekwa moja kwa moja Kijijini kwao Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja kwa mazishi.

Imetolewa na :-
Dk. Juma Mohammed Salum

KNY
Mkurugenzi
Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar
Zanzibar
29, Desemba, 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.