Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Akabidhi Msaada wa Vyarahani.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kulia akipeana mikono ikiwa ni ishara ya kupokelewa na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiangalia nguo ilioshonwa na Wanaushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) mara baada ya kuwasili na kwenda kuangalia maonesho ya Ujasiria mali unaofanywa na Ushirika huo Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.Wanyuma yake ni Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitoa hotuba mara baada ya kukabidhi msdaada wa Vyarahani kwa Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.kulia yake ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico na kushoto yake ni  Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie.
Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie.akitoa hotuba katika sherehe ya upokeaji msaada wa Vyarahani uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kwa kikundi cha Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico akitoa hotuba ya makaribisho katika sherehe ya upokeaji msaada wa Vyarahani uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kwa kikundi cha Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe ya upokeaji msaada wa Vyarahani uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kwa kikundi cha Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kushoto akiwa pamoja na Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie wakikabidhi msaada wa Vyarahani kwa Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozo na Wnaushirika akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.