Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya uteuzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. UTEUZI WA NAIBU KATIBU MKUU

Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake, Vijana na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto. 

2. UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA 

i. Bwana Hemed Suleiman Abdulla ameteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini- Pemba. 

ii. Bwana Hassan Khatib Hassan ameteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini- Unguja.

3. UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MKOA NA WILAYA

i. Bibi Hamida Mussa Khamis ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini/Magharibi.

ii. Bwana Mohamed Abdulla Ahmed ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magharibi “A”.

4. UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

i. Bibi Daima Mohamed Mkalimoto ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika  Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

ii. Bwana Abdulla Issa Mgongo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

5. UTEUZI WA KAMISHNA WA MICHEZO

Bibi Sharifa Khamis Salim ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Michezo katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo.

6. UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MIKOPO YA  ELIMU YA JUU

Bwana Sultan Mohamed Issa Mugheir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya  Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza  tarehe 5 Disemba 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.