Habari za Punde

Rais Dk Shein Aipongeza Timu ya Zanzibar Heroes na Kuwaandalia Chakula cha Mchana Katika Viwanja Vya Ikulu Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco, wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Wachezaji wa Timu hiyo kwa kuonesha mchezo wa hali ya juu na kufikia katika hatua ya Fainali wakati wa michezo ya Kombe la Chalenji Nchini Kenya.
Timu ya Zanzibar Heroes imetolewa kwa njia ya matuta n Timu ya Taifa ya Kenya wiki iliopita na kuchukua nafasi ya Pili ya Michuano hiyo.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Hemed Suleiman Moroco akitowa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa mchango wake katika Sekta ya Soka Zanzibar.

















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.