Habari za Punde

Tanzania Bara yabanwa, Kenya yaanza vyema kombe la Chalenji

 Manahodha wa Timu za Libya na Tanzania bara wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kuanza mchezo wao . Mechi ilimalizika kwa sare ya bila kufungana

Kikosi cha Timu ya Libya ambacho kinashiriki mashindano ya CECAFA kama mwalika kklichomenyana na Timu ya Taifa ya Tanzania Bara , Kilimanjaro Stars


Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.

Wenyeji wa Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP timu ya Taifa ya Kenya wameenza vyema  baada ya leo kuifunga Rwanda mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa saa 8 za mchana katika uwanja wa Bukhungu huko Kakamega .

Mabao ya Kenya yamefungwa na Maasud Juma na Dancon Otieno.

Na katika uwanja wa Kenyata huko Mjini Machakos timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakatoka sare ya 0-0 dhidi ya Libya.

Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Uganda dhidi ya Burundi Saa 9:00 Alaasiri katika uwanja wa Bukhungu huko Kakamega .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.