Habari za Punde

Wapenzi wa Mchezo wa Mpira Kisiwani Pemba na Wachezaji Wamepewa Fursa ya Kushangilia Timu Yao Leo

PEMBA.
CHAMA cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) imehairisha michezo yote ya ligi za madaraja mbali mbali Zanzibar, ili kutoa nafasi kwa wadau na wapenzi wa mpira kuishuhudia timu yao ikicheza fainali ya mashindano ya Chalenji dhidi ya wenyeji Kenya.

Fainali hiyo inayotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, huku Zanzibar Heroes ikiandika historia mpya katika mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, Makamu wa Rais wa ZFA Pemba, Ali Mohamed Ali amesema ZFA imelazikimika kuhairisha, ili wananchi waweze kuishangiria timu yao baada ya kutwaa ubingwa huo.

“sisi hatuna wasiwasi timu itarudi na ubingwa na kumkabidhi Dk Shein, wachezaji wako vizuri wanahamu ya kurudi na ubingwa kama tulivyowakabidhi bendera ya Zanzibar”alisema.

Makamu alisema Zanzibar inajivunia kikosi bora na imara, kinachoongozwa na Kocha mkuu Hemed Moroko na msaidizi wake Hafidh Muhidini,  huku wakiwa na matumaini makubwa ya kutwa ubingwa huo.

Aidha aliwataka wadau wa soka duniani kote kuhakikisha wanaiyombea dua timu ya taifa ya Zanzibar, ili iweze kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Alifahamisha kuwa mwaka 2017 ni mwaka wa kihistoria kwa Zanzibar, kuleta kombe la Chalenji Zanzibar baada ya 1995, huku akiwataka wachezaji kuzidi kujituma.

Nao wadau wa soka kisiwani Pemba wamewapongeza wachezaji na viongozi wa timu kwa hatua waliofikia, huku wakiwataka kuhakikisha wanazidisha ari katika mchezo wa fainali.

Kombo Juma Omar alisema baada ya kurudi nchezi Serikali inapaswa kuwathamini wachezaji kwa kuwaandalia motisha ambayo itakuwa ni historia na kitu watakachokikumbuka katika maisha yao.

Juma Othman Juma alisema ni jambo la busara kwa ZFA kuhairisha ligi zote ili wapenzi wa soka kuitizama timu yao, huku akiwataka wachezaji wengine kujifunza kutoka kwa wachezaji wa timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.