Habari za Punde

NAIBU Waziri wa habari Utalii, Utamaduni na Michezo Aongoza Mazoezi ya Kitaifa Uwanja wa Gombani Pemba na Kuchangia Damu.

NAIBU waziri wa Wizara ya Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar Chumu Kombo Khamis, akiwaongoza Viongozi mbali mbali wa serikali na wanavikundi mbali mbali vya Mazoezi Kisiwani Pemba, ikiwa kila januari mosi ni siku maalumu ya mazoezi kitaifa.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NAIBU Waziri wa habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Chumu Kombo akiwaongoza viongozi mbali mbali wa Serikali katika zoezi la ufanyaji wa mazoezi ya Viungo huko katika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SUALA la Ufanyaji wa Mazoezi sio jambo la watu wazima pekee yao, bali hata watoto nao wanapaswa kufanya mazoezi, pichani kijana akijumuika katika uwanja wa michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

NAIBU waziri wa Wizara ya Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar Chumu Kombo Khamis, akisubiri kupewa majibu yake kutoka kwa madkatari baada ya kupima afya yake, ikiwa ni siku ya mazoezi kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akitolewa sampuli ya damu kuashiria upimaji wa maradhi mbali mbali ikiwemo sukari, wakati wa ufanyaji wa mazoezi katika uwanja wa michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib, akitoa damu kuashiria upimaji wa afya wakati wa ufanyaji wa mazoezi, yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadidi Rashid, akipima presha mara baada ya zoezi la ufanyaji wa mazoezi likimalizaka Ktaika uwanja wa michezo Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ali Salum Matta, akipima presha kwa lengo la kujuwa hali ya afya yake ilivyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.