Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Ashiriki Katika Matembezi ya Tamasha la Tano la Mazoezi January 2018.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Omar Hassan 'King' na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum Mhe. Haji Omar Kheri na kulia Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, wakishiriki katika matembezi ya Tamasha la Tano la Mazoezi Zanzibar wakipita katika mitaa ya Amaan kumalizia matembezi hayo yalioanzia katika Viwanja vya Tumbaku Miembeni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Omar Hassan 'King' na kulia Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, wakishiriki katika matembezi ya Tamasha la Tano la Mazoezi Zanzibar wakipita katika mitaa ya Amaan kumalizia matembezi hayo yalioanzia katika Viwanja vya Tumbaku Miembeni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma , Waziri Kiongozi Mstaaf Shamsi Vuai Nahodha na Mama Asha Shamsi wakiwa wamesimama wakipokea maandamano ya Wanamichezo wakiingia katika Uwanja wa Amaan kwa ajili ya kujumuika katika kufanya mazoezi yalioandalia na Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA)

Brassband ya Jeshi la Mafunzo Zanzibar wakiongoza Matembezi hayo ya Wanamichezo Zanzibar wakiingia katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wanamichezo wakiingia katika Uwanja wa Amaan kumalizia matembezi hayo na kujumuika katika Mazoezi ya pamoja katika uwanja huo. hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1 January. na kuwakutanisha Wanamichezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara. hushiriki katika mazoezi hayo.
Wasanii wa beni wakihamasisha wanamichezo wakati wa Matembezi hayo wakiingia katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Vikundi mbalimbali vya Michezo kutoka Pemba Tanzania Bara na Unguja wakiingia katika viwanja vya Amaan Zanzibar kujumuika katika maadhimisho ya Kitaifa ya Mazoezi hufanyika kila mwaka ifikapo January Mosi.
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakifuatilia mazoezi hayo baada ya kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Kikundi cha Vijana wa Sarakasi kutoka Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja wakitowa burudani ya mchezo huo.

Kiongozi wa Kikundi cha Mazoezi  cha Obama Zanzibar Fatawi Haji akiongoza mazoezi hayo ya Kitaifa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar wakati wa hafla kuadhimisha Siku ya Mazoezi Kitaifa hufanyika kila ifikapo January Mosi na kushirikisha Vikundi vya Mazoezi vya Unguja, Pemba na Tanzania Bara. Huadaliwa na Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) 


Wanamichezo kutoka vikundi mbalimbali wakishiriki mazoezi ya kupanga chupa yaliowashirikisha Wanawake wenye uzito wa kilo mia moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanamichezo  wa Zanzibar katika Tamasha la Tano la Wanamichezo Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar na kuhudhuriwa na Wanamichezo kutoka Tanzania Bara, Pemba na wenyeji Unguja yalioandaliwa na Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) yalioazia katika viwanja vya Matumbaku na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kamishna wa Michezo Zanzibar Bi. Sharifa Khamis akizungumza wakati wa Tamasha la Tano la Michezo Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa Tamasha hilo la Michezo katika Viwanja vya Amaan Zanzibar kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mstaaf Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis,baada ya hafla ya Tamasha la Mazoezi la Kitaifa hufanyika kila mwaka ifikapo January Mosi. hufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kwa kuaza matembezi hayo huazia katika viwanja vya Matumbaku Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.