Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Alizindua Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Soko la Kisasa katika Kijiji cha Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja Lafunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu, Bunge Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, alipowasili katika viwanja vya kinyasini kwa ajili ya ufunguzi wa Soko Jipya la Kisasa Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu Waziri wa Kilimo Mifugo Maliasili na Uvuvi Joseph Abdallah Meza,alipowasili katika viwanja vya kinyasini kwa ajili ya ufunguzi wa Soko Jipya la Kisasa Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mtoto Msikia Rajab Ali aliyeandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo ya uzinduzi wa Soko jipya la kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja kulia Waziri wa Kilimo Mifungo Maliasili na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu. Mhe. Jenista Mhagama
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko hilo Ali Mbarouk, akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wake kutembelea jengo hilo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Soko hilo baada ya kulifungua na akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Mfugo Maliasili na Uvuvi Zanzibar. Mhe. Hamad Rashid Mohammed
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo Maliasini na Uvuvi Joseph Abdallah Meza akitowa maelezo ya kitaalamu ya Ujenzi wa Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi kusherehekea miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu. Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Soko katika Mkoa wa Kaskazini Unguja
WAZIRI wa Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Soko la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar Dk. Shein, kuzungumza na Wananchi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Kai Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati wa hafla hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamad Rashid Mohammed wakati wa hafla hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kaskanizi Unguja wakati wa hafla ya uzinduzi wa Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni shamrashamra za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanziba
WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Soko la Kisasa la Kinyasini Unguja
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.