Habari za Punde

Waziri Amina aweka jiwe la msingi skuli ya Michenzani Wilaya ya Mkoani ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi

WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akisalimiana na Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, Ali Salum Ali Mata mara baada ya kuwasili katika skuli ya Michenzani Wilaya ya Mkoani, kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika skuli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi, banda la vyumba vinne vya skuli ya Msingi michenzani Wilaya ya Mkoani, kushoto ni Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu na na Mafunzo ya Amali Zanzibar Abdalla Mzee Abdalla, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari na Msingi Michenzani Wilaya ya Mkoani, wakimsikiliza kwa makini hutuba ya waziri wa biashara Viwanda na masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika skuli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiangalia ngoma ya Nkota Ngoma ya mkoani, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya msingi Michenzani Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 KATIBU Tawala Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki, akisoma utaratibu wa shuhuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi katika skuli ya Micheweni, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari Michezani Wilaya ya Mkoani, wakiimba wimbo wa mashujaa :SISI SOTE TUMEGOMBA” mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya msingi michenzani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdalla Mzee Abdalla, akisoma taarifa ya kitaalamu ya ujenzi wa banda moja lenye vyumba vine vya kusomea wananfunzi wa msingi Michenzani Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salum Ali, akizungumza na wazazi, walezi, walimu na wanafunzi wa skuli ya Msingi na Sekondari Michenzani Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.