Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu CCM akagua miradi ya TASAF Shehia ya Ndagoni, kisiwani Pemba

 NAIBU katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akiangalia moja ya milango iliyowekwa katika moja ya matuta, yaliyojengwa na Tasaf kupitia kaya masikini Shehia ya Ndagoni, katika Boande la Kagu lenye wakulima zaidi ya 350, ambao miaka ya nyuma walishindwa kulima mpunga.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, mwenye miwani akipiga marufuku wakulima kulima karibu na matuta yaliyojengwa na Tasaf, kupitia kaya masikini shehia ya Ndagoni Wilaya ya Chake Chake, wakati wa ziara ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya CCM 2015/2020.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akichimba msingi wa ujenzi wa tuta la kuzuwia maji chumvi katika bonde la Uchangani, shehia ya Ndagoni Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 BAADHI ya walengwa wa mpango wa kunusuru katika shehia ya Ndagoni, wakichimba msingi wa kujengea tuta kwa lengo la kuzuwia maji chumvi yasivyamie mashamba ya wananchi, katika bonge la Uchangani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akimsikiliza kwa makini mmoja ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini shehia ya Ndagoni, wakati alipotembelea wanakaya hao na kuangalia shughuli zao wanazozifanya.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MRATIBU wa Tassaf Pemba, Mussa Said akijibu maswali ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini, mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk Abdalla Juma Mabodi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Mabodi, akikagua shuhuli za Upandaji wa miti ya Mikandaa, kutoka kwa moja ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akipata maelezo juu ya upangaji wa miti ya mikandaa, kutoka kwa mmoja ya walengo wa kunusuru kaya masikini shehia ya Kukuu Kangani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akimsaidia mmoja ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini, kufunga fundo katika moja ya ncha ya kanga yake ili kuhifadhi fedha alizopatiwa na chama cha Mapinduzi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akimkabidhi fedha mmoja ya wanakikundi cha usukaji na upakaji wa rangi shehia ya Mtangani, wakati wa ziara yake ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya CCM 2015/2020. .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.