Habari za Punde

Walimu 16 Kati ya 39 wa Masomo ya Hesabati na Fizikia Kutoka Nchini Nigeria Wawasili Zanzibar Leo Kufundisha Masomo Hayo Kwa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba.

Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria Wawasili leo kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia wakiwa na Mkurugenzi Program Mr. J.A.Oduniyi, jumla ya Walimu wa masomo hayo 16 wamewasili kati ya 39 wanaotarajiwa kuja zanzibar kufundisha masoma hayo, kwa Skuli za Sekondari Zanzibar. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wamepokelewa na Afisi wa Elimu Sekondari Mwalimu Khalifa Rashid.  
 Afisa Elimu Sekondari Zanzibar Mwalimu Khalifa Rashid akisalimiana na Mkuu wa Msafara wa Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria Mr. J.A Oduniyi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea Nchini Nigeria kwa ajili ya kuja kufundisha Wanafunzi wa Skuli za Unguja na Pemba za Sekondari Jumla ya Walomu 39 wanatarajiwa kuwasili Zanzibar leo wamewasili Walimu 16. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.