Habari za Punde

Ziara ya Makamishna wa kamisheni ya Utalii kisiwani Pemba

 MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali, akitoa historia fupi ya Utalii kwa Wilaya ya Wete na Micheweni, wakati wa ziara ya Makamishna wa kamisheni ya Utalii Zanzibar, huko katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 KATIBU Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ahmed Khalid Abdalla akizungumza katika kikao cha pamoja na Makamishna wa kamisheni ya Utalii Zanzibar, huko katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MSHAURI wa Rais Pemba Dk Mauwa Abeid Daftari, akizungumza katika kikao cha Pamoja na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, huko katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman akizungumza na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wakati makamishna hao walipofika katika ofisi hiyo kujitambulisha kwake na kuzan ziara yao ya siku mbili Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

 KATIBU mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk Vuai Iddi Lila, akiwasilisha mapendekezo na michango ya Kamisheni ya Utalii, kwa Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati makamishna wa kamisheni ya utalii Zanzibar walipofanya ziara mkoa huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
MWENYEKITI wa kamisheni ya Utalii Zanzibar Sihaaba Saleh, akizungumza katika kikao cha pamoja na makamishna wa kamisheni ya utalii Zanzibar na uongozi wa serikali ya mkoa wa kaskazini Pemba, wakati wa ziara ya siku mbili kwa makamishna wa kamisheni hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.