Habari za Punde

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA UKAGUZI WA VIFAA VYA KINGA NA TAHADHARI, DHIDI YA MOTO NA KUTOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO VYA HUDUMA YA KWANZA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM.


 Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Edgar Mwakapala akionesha jinsi ya kuzima moto kwa kutumia blanket maalumu la kuzimia moto kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala iliyopo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wakati wa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto mapema leo asubuhi.
Mmoja kati ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala akifanya mafunzo ya kuzima moto kwa vitendo kwa kutumia kizimia moto  chenye mchanganyiko wa maji na povu (Foam) wakati wa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lafanya  ukaguzi wa vifaa vya kinga na tahadhari dhidi ya moto pamoja na kutoa mafunzo ya matumizi ya vifaa vya kuzimia moto vya huduma ya kwanza katika Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.