Fatma Makame - Maelezo Zanzibar
Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar ikishirikiana na Radio Adhana imekabidhi Misahafu 1,200 kwa Wanafunzi wa Skuli nne za Jimbo la chwaka Wilaya ya kati mkoa wa Kusini Unguja ikiwemo SKuli ya Chwaka,Marumbi, Pongwe na Koani.
Msaada wa Misahafu hiyo una lengo la kuwapatia Wanafunzi hao fursa ya kujifunza zaidi Dini ya kiislamu kupitia Misahafu hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kukabidhi Misahafu hiyo Mwenyekiti huduma kwa jamii Jumuiya ya istiqaka Zanzibar Said Hamed Haroub amesema lengo la kuwapatia Misahafu hiyo ni kuisoma na kuwa mwongozo wa maisha yao ya Dunia na akhera.
Amesema si vyema Misahafu hiyo kupuuzwa kwa kuifungia ndani badala yake wanatakiwa kuipa umuhimu katika maisha yao ya kila siku.
Amesema Wanafunzi hao wanapswa wakipe umuhimu Mkubwa kitabu hicho kitukufu kwa vile wanapokisoma kitachochea ufahamu mkubwa kwa masomo yao ya kawaida.
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wanafunzi wa skuli ya chwaka kuitumia vizuri misahafu hiyo na kuyafata yale yaliyo amrishwa ndani ya kitabu hicho na kutoyafanya yasiyo ya maana katika uislamu kwa kukabidhi misahafu elfu moja miambili 1200 .
Kwa upande wake nae Naibu Mkurugenzi wa Radio Adhana Said Suleiman amewataka wanafunzi hao kuisoma kur-ani kwa ajili ya kuchuma thawabu na kujijengea maisha yenye kufuata mwongozo sahihi ya dini ya kislamu .
Nae Mwalimu mkuu wa skuli ya chwaka Tatu Shaabani Mayala ametowa shukrani kwa Jumuiya ya istikama kwa kuwapatia misahafu ambayo itakuwa kichocheo ya kuimarisha maadili mema ya Wanafunzi hao.
Amewahimiza Wanafunzi hao kukisoma Kitabu hicho na kurudi Chuoni kwa wanafunzi ambao wametoroka Vyuoni ili kuifahamu vyema dini yao.
Awali Diwani wa wadi ya Chwaka Mlenge Khatibu Mlenge ameipongeza jumuiya hiyo misaada hiyo ya kitabu cha Qur –ani na kuwataka wanafuzi kukitunza na kuvisoma vizur kwani ndicho chimbuko la elimu.
Imtolewa na Maelezo Zanzibar
No comments:
Post a Comment