Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa
Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Emmanuel Baudran.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamefanyika
Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi Clavier amewasilisha salaam za Rais
wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kusema
“Rais wa Ufaransa ana uhakika na Tanzania ijayo na anaunga mkono
jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli”
Balozi huyo mpya wa Ufaransa nchini ambaye
amekutana na kuzungumza na Mheshimiwa Makamu wa Rais aliipongeza Tanzania kwa
kuwa mstari wa mbele katika masuala mbali mbali ya Kimataifa na kusema
“Tanzania ni nchi yenye utulivu na Amani
kitu ambacho kinaipa taswira nzuri Umoja wa Mataifa”.
Mhe. Balozi amemjulisha Makamu wa Rais
kwamba Ufaransa imekusudia kuimarisha uhusiano zaidi na Tanzania wa Uchumi na
Siasa na kuanzisha majadiliano mbali mbali katika masuala ya Mazingira,Mabadiliko
ya Tabia Nchi.
Balozi Clavier amemjulisha Makamu wa Rais
kuwa mwezi ujao kutakuwa na ugeni wa wafanya biashara kati ya 30 au 40 kutoka
nchi ya Ufaransa ambao watakuja kujionea fursa mbali mbali za kibiashara na
uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Mhe. Balozi amemuelezea Makamu wa Rais azma
ya Ufaransa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Tanzania katika kuanzisha na
kuendesha kozi mbali mbali kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mwisho aliipongeza Serikali kwa mapambano
dhidi ya rushwa na urasimu jambo litakalo wavutia wawekezaji wengi nchini.
Aidha, Bw. Emmanuel Baudran Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa alisema Shirika lao linakusudia kuanzisha kiwanda
cha vifaa vya umeme wa jua (solar) mkoani Shinyanga pia shirika hilo
limeshafanya miradi ya uboreshaji maji taka katika manispaa ya Temeke na
wanaendelea na mikakati ya uanzishwaji wa miradi mingine.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimshukuru na kumpongeza Balozi
wa Ufaransa kwa kazi nzuri wanazofanya hapa nchini.
Alimhakikishia kwamba Serikali ya Tanzania
ipo tayari kutoa ushirikiano kwa mambo yote muhimu yenye maslahi kwa wananchi.
Wakati huohuo Makamu wa Rais alikutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Mhe. Michael Danford.
No comments:
Post a Comment