Habari za Punde

RC Kusini Pemba atoa tahadhari ya mvua za Masika


Taarifa kwa Umma.

Kutokana na kipindi cha mvua tunachokiingia hivi sasa , natoa wito kwa wananchi wote wa Zanzibar hususan wa mkoa wa kusini Pemba kuchukua tahadhari ya hali ya juu katika mvua hizo.

Pamoja na hayo pia natoa wito kwa wale wote wanaoishi sehemu za mabondeni, kuanzia sasa watafute namna ya kuhama katika maeneo hayo kwani mvua zinapokuja hasa hasa huathiri maeneo hayo, ingawa hali ni nzito lakini jitahidini na hili ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.

Sambamba na hayo, wananchi wadumishe usafi wa mazingira katika maeneo yao ya na makaazi ili kujiepusha na maradhi ya mripuko yanayoweza kujitokeza iwapo mazingira hayatokua safi.

Kupitia wito huu natumai wananchi mutauitikia vizuri , lengo ni kujiepusha na madhara kwani gharama zake ni kubwa yanapokufika.
Nakupendeni sana wananchi wangu.

Kutoka : Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba
              Hemed Suleiman Abdalla


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.