Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya kulia akiwa na wajumbe wenzake .
Na. MatukiodaimaBlog.
SHIRIKISHO la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao ni waandaaji wa sherehe za wafanyakazi kitaifa (MEI MOSI) wamempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa .
Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya alisema leo kuwa katika sherehe hizo za wafanyakazi duniani kwa Tanzania zitafanyika katika mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa Samora na kuwa tayari Rais Dkt Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi .
Hivyo aliwataka wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe hizo na kuwa kupitia sherehe hizo watapata fursa ya kujua mikakati ya serikali dhidi ya wafanyakazi nchini japo hadi sasa wanapongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya kuwarejesha kazini wafanyakazi waliokuwa wamesimamishwa kazi kutokana na elimu yao ya darasa la saba.
Rais huyo alisema kuwa TUCTA imefanya jitihada kubwa za kukutana na serikali kuwapigania wafanyakazi hao walioondolewa kazini kutokana na elimu yao na serikali imesikiliza na imewarejesha kazini .
Alisema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa kuongeza ajira pamoja na kusikiliza kero mbali mbali za wafanyakazi na kuzipatia majibu .
Akielezea juu ya maandalizi ya sherehe za mei mosi mkoani Iringa alisema kwa sehemu kubwa maandalizi yanakwenda vizuri na wamepata ratibu ya kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Iringa kutoa elimu pamoja na kututana na wafanyakazi ili kujua changamoto zao.
" TUCTA inapenda kuishukuru serikali ya mkoa wa Iringa kwa kukubali kupokea maadhimisho haya ya Mei mosi 2018 TUCTA kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza pamoja na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge ,kazi ,vijana , ajira na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama tumefanya maandalizi ya kutosha"
Alisema kabla ya Mei mosi mambo yakayofanyika Iringa ni pamoja na makongamano mawili ya kimkoa na moja la kitaifa na kuwakongamano la kwanza litafanyika April 23 katika wilaya ya Mufindi ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam wakati kongamano la pili litafanyika wilaya ya Kilolo April 25 na mgeni rasmi ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah huku April 27 litafanyika kongamano la kitaifa litakalohusu Tanzania ya uchumi wa viwanda kwenye ukumbi wa Kichangani ambalo viongozi mbali mbali wa kitaifa watashiriki .
Aidha alisema kutakuwa na michezo ya Mei mosi ya fani mbali mbali itakayoanza April 16 hadi April 30 katika uwanja wa Samora kuwa kwa ajili ya kuwafanya wafanyabiashara na wajasilia mali kutumia fursa ya mei mosi Iringa maonyesho ya bidhaa mbali mbali yatafanyika .
|
No comments:
Post a Comment