Habari za Punde

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA POLISI JIJINI ARUSHA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro  wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na viongozi wengine pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya familia za askari polisi baada ya kufungua  rasmi nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 

Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.