Habari za Punde

TAARIFA YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KWA UMMA-KUFUATIA TUKIO LA MOTO KWENYE UKUMBI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


                                               JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                 JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
9 Barabra ya Ohio
  S. L. P. 5821,
  DAR ES SALAAM.
 

Simu ya maandishi: “ZIMAMOTO KUU”
Simu Nambari:  +255-22-2113537
Nukushi:          + 255-22-2184569
Tovuti : www.frr.go.tz

                                                                                                  


     TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia tukio la moto kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotokea mnamo tarehe 09 Aprili, 2018 majira ya saa 1:28 usiku mkoani Dodoma.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na shoti iliyotokana na Power bank iliyokuwa inatumiwa kuchaji simu. Shoti hiyo ilisababisha kuungua kwa simu, Power bank, sehemu ya meza na kapeti kitendo kilicholeta moshi mkubwa na taharuki miongoni mwa Wabunge. Ukiachilia mbali taharuki kwa Waheshimiwa Wabunge hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokana na moto huo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa rai kwa Watanzania wote kuchukua tahadhari kubwa hasa wanapokua wanatumia vifaa vya kieletroniki ambavyo kwa sasa vipo katika matumizi hadi katika ngazi ya familia. Moto huzuka tu endapo kitapatikana chakula cha moto, joto la kutosha na hewa ya oksijeni (fuel, heat and oxygen).

Sambamba na hayo Kamishna Jenerali anahimiza uzingatiaji wa kinga na tahadhari ya moto katika maeneo yote. Wamiliki wa maeneo ya umma, binafsi na biashara wanapaswa kufunga vizimia moto kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lipo imara na litaendelea kuwaelimisha Watanzania kuzingatia kinga na tahadhari ya moto ili kuhakikisha maisha na mali vinakuwa salama.
Imetolewa na;
   

CGF. Thobias Andengenye
Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
10 Aprili, 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.